CHAMA CHA KISWAHILI AFRIKA MASHARIKI (CHAKAMA)

Historia
Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) ni chama cha wahadhiri wa Kiswahili wa vyuo vikuu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Chama hiki kilizinduliwa tarehe 7 Julai mwaka 2002 na wajumbe wa warsha ya wataalamu wa Kiswahili wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki wakati wa  mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Eland, Arusha, Tanzania.
Lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hiki lilikuwa kukuza Kiswahili na kuvileta pamoja vyuo vikuu vya Afrika Mashariki.
Viongozi wa awamu ya kwanza waliochaguliwa katika mkutano wa Arusha walikuwa ifuatavyo:

 1. Mwenyekiti- Prof. Naomi Shitemi (Kenya)
 2. Katibu Mkuu- Dkt. Inyani Simala (Kenya)
 3. Mhazini- Dkt. I.H. Ziddy (Zanzibar)
 4. Naibu Mwenyekiti- Prof. David P.B. Massamba (Tanzania)
 5. Naibu Katibu Mkuu- Dkt. John D. Kiango (Tanzania)
 6. Naibu Mhazini- Dkt. Clara Momanyi (Kenya)
 7. Afisa Ushirikiano- Prof. Kimani Njogu (Kenya)
 8. Afisa Uenezi- Dkt. Aldin Mutembei (Tanzania)

Viongozi wa matawi ya CHAKAMA waliochaguliwa mwaka huo walikuwa wafuatao:
 
Kenya

 1. Mwenyekiti- Dkt. Catherine Ndungo
 2. Katibu- Dkt. Karisa Beja

 
Tanzania

 1. Mwenyekiti- Bi. E. Mosha
 2. Katibu- Dkt Yohana Msanjila

Uganda

 1. Ruth Mukama
 2. Austin Bukenya

Viongozi wa awamu ya pili waliochaguliwa Machi 30 mwaka 2006 walikuwa:

 1. Mwenyekiti – David P.B. Massamba (Tanzania)
 2. Naibu Mwenyekiti- Dkt. John Nsookwa (Uganda)
 3. Katibu Mkuu- John D. Kiango (Tanzania)
 4. Naibu katibu Mkuu- Dkt. Innocent
 5. Mhazini- Dkt. Clara Momany (Kenya)
 6. Naibu Mhazini- Bw. Amour Hamisi (Zanzibar)
 7. Mhariri Mkuu- Prof. Fumikeni M. K. Senkoro (Tanzania)
 8. Katibu Uenezi- Dkt. Aldin Mutembei (Tanzania)
 9. Katibu Uhusiano- Bi. Mwanakombo Noordin (Kenya)

Baadhi ya mafanikio ya mwanzo ni pamoja na:

 1. Kuanzisha Jarida la CHAKAMA
 2. Kuandika katiba ya CHAKAMA
 3. Kubuni Logo ya Chama
 4. Kuunda kamati za Chama
 5. Kuandika pendekezo la Shule ya Upili ya CHAKAMA ( inayotoa mafunzo yote kwa Kiswahili)
 6. Kukisajili Chama rasmi.
 7. Kuchapisha kumbukizi za wataalamu wa Kiswahili waliotangulia mbele ya haki.
 8. Kuanzisha Chama cha wanafunzi cha CHAWAKAMA ( Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki)

Wanachama walifaidika kwa namna nyingi kama vile:

 1. Kukutana na kufahamiana na wataalamu wengine
 2. Kujitangaza

Maelezo ya kuwaenzi wataalamu waliopo na waliotangulia mbele ya haki

Ni muhimu kutaja kuwa wakurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam  waliwajumuishwa kwenye uongozi wa CHAKAMA. Katika awamu ya kwanza Mkurugenzi alikuwa Prof. Mugyabuso Mulinzi Mulokozi.

Mwanzoni mikutano na makongamano yalifanyika Arusha kwa sababu ya ukati wa mji huo. Baadaye shughuli hizo zikawa zinafanyika katika nchi iliyotwaa uongozi. Mwaka 2009 ikawa Kampala, Uganda;  2011 – Nakuru, Kenya; 2013 – Mwanza, Tanzania; 2015 – Thika, Kenya; 2017 – Dodoma, Tanzania na 2019 – Narok, Kenya.
Hata hivyo, Kongamano la mwaka 2005 lilifanyika katika mji wa Eldoret, Kenya.

Wenyekiti wa CHAKAMA wa baadaye: 2009 -2011- Dkt. Prof. Isaac Ipara Odeo (Kenya); 2011 – 2013  – Dkt. E. Chiduo (Tanzania); 2013 – 2015 – Prof. Ernest Sangai Mohochi (Kenya); 2015 – 2017 – Dkt. Mussa Hans (Tanzania); 2017 – 2019 – Dkt. James Ontieri (Kenya) na 2019 –  – Bi. Aidah Mutenyo (Uganda).